▼▼▼TO SEE PHOTOS AND THE VIDEO CLICK HERE DOWN▼▼▼
Serikali imesema inakamilisha taratibu za kuanzisha mfumo wa ulinzi wa raia na mali zao kwa njia ya mtandao wa kamera za usalama, ikianza na Mkoa wa Dar es Salaam kwa mwaka ujao wa fedha.
Aidha, itakamilisha taratibu za kuanzisha ukaguzi wa lazima wa magari yote nchini pamoja na taratibu za ufuatiliaji wa magari yaendayo mikoani kwa njia ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama).
Sambamba na hilo, katika kusaidia kudhibiti ajali za barabarani, Jeshi la Polisi lina mpango wa matumizi ya mfumo wa pointi na ufungaji wa kamera za kudumu za barabarani.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga aliyasema hayo bungeni mjini hapa jana wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2016/17.
Kitwanga alisema ufungaji wa kamera za usalama (CCTV) utaanzia katika Mkoa wa Dar es Salaam katika mwaka ujao wa fedha na kisha kuhamia mikoa mingine nchini. Alisema katika mwaka huo, polisi itaanza rasmi kutekeleza Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) katika Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni kama sehemu ya kuboresha utendaji na kuimarisha usalama wa nchi.
“Inatarajiwa kuwa mpango huu utatekelezwa nchi nzima baada ya kubaini changamoto zitakazotokana na utekelezaji huo katika Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni,” alisema Kitwanga
Post a Comment